send link to app

Momoa


4.6 ( 6736 ratings )
Finanzas Economía y empresa
Desarrollador erick Justin Nyaluke
Libre

Momoa ni app inayomuwezesha wakala kutunza taarifa za miamala yake. Badala ya kurekodi miamala kwenye karatasi au kutorekodi, sasa wakala ataweza kutunza taarifa hizo kwenye simu.

Kupitia app ya Momoa:
Wakala anaweza kurekodi miamala ya kuweka pesa (Ambapo anakua kapokea cash)
Wakala anaweza kurekodi miamala ya kutoa pesa (ambapo wakala ametoa cash na kumpatia mteja)
Wakala anaweza kurekodi muamala kama ni deni (madeni ni pale mteja hajachukua hela yake au wakala hajapewa hela yake na mteja)
Wakala anaweza kurekodi muamala kwa kumuainisha mteja kwa jina au namba ya simu
Wakala atakua anaweza kuthibitisha hesabu zake wakati anavoanza siku na wakati anapofunga kwa urahisi, na kuweza kuona kama hesabu zimebalance au laa.
Wakala anaweza kuangalia historia au ripoti ya nyuma ya miamala yote, hesabu alivoanza na alivofunga siku.
Wakala anaweza kuedit float au Cash. Hii ni kusaidia kama karushiwa float na wakala mwenzake au kafanya muamala kwa njia ya bank.
Wakala anaweza kuongeza mtandao au bank kwa kadri ya awezavyo, na atatakiwa kujaza float iliyopo katika kila mtandao.

Tunawapenda mawakala na tuna matumaini Momoa itawasaidia kuzikuza biashara zao na kufanya usimamiaji uwe mwepesi, rahisi na haraka.

Karibu Momoa. Kama unakitu unatamani tuboreshe au kuongeza tunaomba uwasiliane na sisi kupitia namba +255 682 411 725 (call or whatsapp)